Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina Lake Aliyetukuka
Kwa heshima kubwa kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya juu waliopo katika tafiti za Hawza,
Baada ya salamu na maamkizi, pamoja na kutakieni ushindi na ufanisi mashujaa na wenye nyoyo jasiri wa kambi ya haki dhidi ya batili;
Sasa ambapo kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, ishara za kudhihirika kwa irada ya Mwenyezi Mungu katika ushindi na nusra ya jeshi la Mwenyezi Mungu, na kudhalilika na kushindwa kwa nguvu za kiburi cha dunia na Uzayuni wa kimataifa zimeonekana wazi;
Inafaa watu wote kushiriki katika harakati hii ya pamoja ya uwepo, na kila mtu, hasa wanazuoni wakubwa wa dini, wawe na mchango mkubwa zaidi katika kutekeleza majukumu yao ya Kimungu.
Kwa msingi huo, tafiti za kielimu zimeathiriwa na harakati hii ya Kimungu, na hadi taarifa nyingine itakapo tolewa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidishe mafanikio na ushindi kwa Ummah na mfumo wa Kiislamu.
Abdullah Jawadi Amoli
14 Farvardin 1405
Zingatia: Inaarifiwa kwamba masomo ya Mtukufu Ustadh yamesimamishwa hadi taarifa nyingine itakapo tolewa.
Maoni yako